88 views 25 secs 0 comments

UHAMISHAJI NA WADAU KUTOA ELIMU YA MAZINGIRA

In KITAIFA
May 28, 2023
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis amevitaka taasisi na wadau wa mazingira wa mazingira kuendelea kutoa elimu kuhusu umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Khamis Hamza Khamis
amevitaka vyombo vya habari, taasisi na wadau wa mazingira wa mazingira
kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji na uhifadhi
wa mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza leo Mei 26, 2023 wakati wa hafla ya zoezi la upandaji miti katika
Shule ya Sekondari Buigiri iliyopo Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino jijini
Dodoma, Naibu Waziri Khamis amesema suala la uhifadhi wa mazingira ni jambo
mtambuka linalohitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali.
Mhe. Khamis amesema viongozi wakuu wa dunia kila wakutanapo katika vikao na
mikutano mbalimbali hujadili kwa kina masuala muhimu ya kidunia ikiwemo
ajenda ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira ambapo umuhimu wake unabeba
mustakabali wa viumbe hai, rasilimali na maliasili zilizopo katika uso wa dunia.
โ€œMabadiliko ya tabianchi ni ongezeko la muda mrefu la joto la wastani la dunia
na kusababisha kubadilika kwa mfumo mzima wa hali ya hewa, ili kuinusuru jamii
yetu kutoka kwenye changamoto hizi tunapaswa kupanda miti kwa wingi ili
kuokoa maisha ya viumbe hai wengine pamoja na binadamuโ€ amesema Naibu
Waziri Khamis.

/ Published posts: 1414

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram