223 views 57 secs 0 comments

MWANAMITINDO MTANZANIA KUITANGAZA ADIDAS DUNIANI.

In Uncategorized
July 13, 2023

Kampuni ya mitindo ya mavazi inayomiliki chapa ya Adidas imeingia mkataba wa matangazo ya mitindo ya mavazi na Mwanamitindo kutoka Tanzania, Zuhura Bedel Said maarufu Zara. Zara anayetoka Zanzibar ameingia mkataba huo hivi karibuni baada ya kuwepo kwenye kumi bora, ambapo ataitangaza chapa ya Adidas kupitia mitindo ya mavazi.

Habari hiyo ilithibitishwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo ambaye alizungumza kwa njia ya simu na TBCOnline.

Wanamitindo wengine tisa wanatoka katika jiji la Milano nchini Italia, jiji linalofahamika sana kwa mitindo ya mavazi kutokana na kuwepo kwa kampuni kubwa za mitindo kama Gucci, Valentino na Armani.

Amesema juhudi hizo za Rais Samia zimerahisisha kazi za Mabalozi kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram