Kufuatia tukio alililolifanya Mwalimu Sabina Haule kutoka shule ya Sekondari Loleza la kuwalaza wanafunzi Darasani na kupelekea Mkuu wa Mkoa kumuagiza Afisa Elimu kumchukulia hatua Mwalimu huyo hatimae hii leo RC Homera ametangaza kumsamehe Mwalimu huyo na kumtaka achape kazi kwa bidii na kurekebisha baadhi ya changamoto.
RC Homera ametangaza msamaha huo baada ya Mwalimu Haule kumtembelea ofisini kwake na kumuomba msamaha na kuahidi kutorudia kosa badala yake atahakikisha anakuwa Mwalimu mwema kwa Wanafunzi.
Akizungumza baada ya kupewa nafasi Sabina Haule ambaye ni Mwalimu wa Mabweni shuleni Loleza amekiri kufanya kosa lile na kuongeza kuwa yeye ni Mwanadam Mapungufu anayo atakachofanya sasa hivi baada ya kupewa nafasi nyingine na RC Homera ni kujitahidi kutorudia kosa badala yake atajikita katika kutimiza wajibu wake jwa shule na Taifa kwa Ujumla Alisema Madam Haule.
Aidha amempongeza RC Homera kwa kuwa na roho ya Ubinadam na usikivu na kuahidi kuufanyia kazi ushauri na mambo mengine yoote ambayo amemuelekeza.
Ikumbukwe Usiku wa tarehe 11 kuamkia 12 Mwalimu Haule alitenda kosa la kuwalaza Darasanj Wanafunzi wa shule ya Wasichana Loleza makusudi na kuondoka na ufunguo jambo lililopelekea RC Homera kufika shuleni hapo na kutoa maelekezo
Chanzo: Access Fm