Jeshi la Marekani na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamezindua mafunzo ya pili ya pamoja ya kila mwaka katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Kunduchi Tarehe 21 Julai 2023.
Mafunzo haya yatafanyika sehemu mbalimbali Tanzania katika kipindi cha miezi michache ijayo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya vikosi maalum vya Majeshi ya Marekani na Tanzania vinavyosaidia mchango wa Tanzania katika oparesheni za kulinda amani katika kanda. Ushirikiano wa kiusalama kati ya 🇺🇸 na 🇹🇿 umeendelea kuwa imara, na kama alivyoeleza Balozi wa Marekani nchini Tanzania Michael Battle, “Tanzania ina washirika wengi katika masuala ya usalama, lakini Marekani itajitahidi kuwa mshirika wenu bora zaidi.