949 views 58 secs 0 comments

MSANII HAITHAM KIM AFARIKI DUNIA.

In BURUDANI, KITAIFA
September 01, 2023

Msanii wa Bongofleva Haitham Kim ambaye hivi karibuni Wasanii na Wadau wengine mbalimbali walianzisha kampeni ya kusaidia kuchangisha pesa kwa ajili ya matibabu yake amefariki leo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke Jijini Dar es salaam.

BNB ambaye ni Rafiki wa Mume wa Marehemu Haitham, ameithibitisha kuwa ni kweli Haitham amefariki leo Hospitalini hapo.

Katika mahojiano na moja ya chombo cha habari Bryson ambaye ni Mume wa Marehemu alisema hali ya Haitham ilibadilika ghafla siku saba zilizopita akisumbuliwa na upumuaji ambapo ilianza kama homa ya kawaida lakini baadaye akawa anakosa pumzi hadi kupelekea kuwekewa mashine na kuchomwa sindano za kila siku zinazogharimu shilingi laki 7 kwa siku.

BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

Editor / Published posts: 21

Journalist

Twitter
Facebook
Youtube
Linkedin
Instagram