145 views 2 mins 0 comments

RC CHALAMILA BARABARA NYINGI ZIME ATHIRIKA KUTOKANA NA UZEMBE WA CHINI WA KIWANGO

In KITAIFA
May 28, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema barabara nyingi zime athirika wakati wa mvua na hii inatokana na barabara zilizotengenezwa Kwa uzembe Chini ya kiwango na zengine hazina mitaro na ujenzi wa wananchi waliojenga umeziba njia ya maji

Hayo ameyasema Leo Tarehe 28 Mei 2024 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila Amesema Maji yakiwa machache yanaweza kupiga Kona yenyewe lakini yakijaa hayana Muda wa Kona yatapasua katikati ya majenzi ya watu



Aidha Chalamila ametoa Lai na kusema mara baada ya ukarabari wa ujenzi utakapoanza kila mtanzania wa kawaida ajitambue mwenyewe usisubili nguvu ya serikali ije ikuelekeze

“hapa bomoa hapa acha wewe mwenyewe chukua hatua rudisha kidogo ukuta wako Ili maji yaweze kupita kirahisi usichofanya kitu kama hicho tutakuelimisha Kwa mara ya kwanza na mara ya pili na mara ya tatu mara ya Nne tutachukua jukumu la kubomoa Kuta Ili maji yaweze kupita Kwa sababu ni muhimu kutunza rasilimali ya barabara Ili tusitengeneze mara Kwa mara ni muhimu pia kulinda maisha ya watu Ili maisha yenu yaweze kwenda vizuri”Amesema Chalamila



Aidha Mkuu wa Wilaya ya ilala Edward Mpogolo Nae Amebainisha kuwa barabara hii inapita kata Tano kitunda,kivule, msongola,kata ya mzinga na Temeke na wote Kwa pamoja wanatumia hii barabara Kwa huduma za kijamii na hospital ya Wilaya

“Mhe Rais ameleta ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inayoenda kujengwa shule hiyo ya gorofa yenye thamani ya shilingi Bilioni 100 na milioni 800 kwahiyo Kuna kazi kubwa ya Rais anaifanya”Amesema Mpogolo



Nae Diwani wa kata ya kitunda Victar Kagombora Amesema Kuna changamoto kubwa ambayo IPO Kwa mda mrefu ya barabara ya kutoka banana,kitunda,kivule na kwenda msongora barabara hii imeekwa Katika ilani ya uchaguzi 2015/2020 bahati mbaya barabara haikuweza kujengwa pia imeekwa Katika ilani ya uchaguzi 2020/2025

“Wewe ni mteule wa Rais tunajua unamfikia haraka tunamuomba Kwa Niaba ya wananchi wa kata ya kivule, Msongora na kitunda, barabara hii itafanya kura za Mhe Rais ziwe chache pia mbunge wetu Jerry slaa anaweza kukosa kula kama barabara hii haitajengwa Na Mwiba ambao utakaoweza tushinde ni barabara hii kujengwa”Amesema Kagombora

/ Published posts: 1440

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram