169 views 42 secs 0 comments

DKT NCHIMBI AZINDUA SHINA LA WAKEREKETWA WAJASIRIAMALI WA TARIME GROUP

In KITAIFA
June 02, 2024
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi asisitiza watendaji wa Serikali kuwa na uchungu wa fedha za umma usimamizi wa miradi ya maendeleo, waendane na kasi ya Mhe. Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi akizindua Shina la Wakereketwa Wajasiriamali wa Tarime Group, lenye wanachama 200, eneo la Makuyuni, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.

Balozi Nchimbi amewasili na kupokelewa Arusha leo Jumapili, Juni 2, 2024, tayari kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake kwenye mikoa mitano, ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, akiwa amembatana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA. Amos Makalla pamoja na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Hamid Abdallah.

Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, ukipokelewa katika eneo la Mijingu, Mkoa wa Arusha, Jumapili Juni 2, 2024, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo, baada ya kumaliza ziara katika Mkoa wa Manyara. Balozi Nchimbi ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Komredi Rabia Hamid Abdalla.

/ Published posts: 1414

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram