173 views 20 secs 0 comments

RUHSA VYAMA VYA SIASA KUWEKA MAWAKALA UBORESHAJI WA DAFTARI

In KITAIFA
June 08, 2024

Na mwandishi wetu WAMACHINGA

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji (Rufaa), Jacobs Mwambegele akikabidhi nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura kwa viongozi na wawakilishi wa Vyama 19 vyenye usajili kamili wakati Vyama hivyo vilipokutana katika mkutano wa Tume na viongozi wa vyama vya siasa uliofanyika jijini Dar es Salaam leo tarehe 07 Juni, 2024 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari.



Mapema wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Jaji Mwambegele aliahidi kuvipatia nakala hiyo vyama vyote na pia Vyama hivyo vitapatiwa nakala tepe ya orodha hiyo



“Leo kila chama kitapewa nakala ya orodha ya vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura. Dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura,” amesema Jaji Mwambegele.



Vyama hivyo vilivyopokea ni AAFP, ACT – WAZALENDO, ADA – TADEA, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CHAUMA, CUF, Demokrasia Makaini, DP, NCCRA- MAGEUZI, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD na UPDP.

/ Published posts: 1435

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram