Na Mwandishi wetu WAMACHINGA KENYA
Baada ya siku ya maandamano, ghasia na umwagaji damu, Rais wa Kenya William Ruto alihutubia taifa kwa ujumbe wa huzuni na wenye nguvu.
Akisema maandamano “halali” dhidi ya sera zake “yametekwa nyara na kundi la wahalifu waliopangwa,” alionya serikali yake itatumia njia zote ili kuzuia kujirudia kwa ghasia hizo, “kwa gharama yoyote”.
“Matukio ya leo yanaashiria hatua muhimu ya jinsi tunavyokabiliana na vitisho vya amani yetu,” alisema. “Tutahakikisha hali ya aina hii haijirudii tena.”
Ujumbe wa rais ulikuwa jaribio la kunyakua udhibiti baada ya siku kadhaa za maandamano ya mitaani ambayo yameongezeka kwa nguvu. Siku ya Jumanne, waliongezeka huku watu wasiopungua watano wakipigwa risasi na mamia kujeruhiwa.
Lakini kwa muda mrefu baadhi ya watu wa Bw. Ruto lazima wahofu kwamba huenda mambo yasiwe rahisi sana, na kwamba bado kuna hatua ngumu za kuchukua siku za usoni.
Alipochaguliwa mwaka wa 2022 aliahidi kupunguza ufisadi, kuinua uchumi wa nchi unaodorora na kusaidia maskini, Lakini Bw Ruto sasa anakabiliwa na uasi usio na kifani dhidi ya muswada anaosema kuwa ni sehemu muhimu ya mpango wake wa kujenga taifa.
Huenda ikawa rahisi kujua ni hatua gani angechukua iwapo upinzani anaokabiliana nao Bw.Ruto ungesalia ndani ya bunge.
Akiwa mwanasiasa mahiri, na naibu rais kwa takribani muongo mmoja kabla ya kuchaguliwa, Bw Ruto ana tajriba ya miaka mingi akizozana kisiasa ili mambo yafanyike.
Lakini sasa nguvu zilizokusanyika dhidi yake ni kitu asichoweza kukidhibiti.
Vuguvugu la kutoridhika lililooneshwa kwenye mitandao ya kijamii sasa limebadilika na kuwa upinzani mkubwa ambao umejaza mitaa ya miji kote nchini.
Katika mji mkuu, ofisi ya gavana wa Nairobi, sehemu ya Jengo la bunge la kaunti ya Nairobi, na jengo la bunge la nchi hiyo yaliharibiwa kwa moto.
Waandamanaji walikuwa wameanza siku hiyo wakitishia “kufunga kabisa nchi”.
Na mwisho wa siku ya machafuko na hofu nchini kote, mara nyingi dhidi ya sauti ya gesi ya machozi na wakati mwingine risasi za moto kutoka kwa polisi, bila shaka hasira yao imesikika.
Kujibu, Bw Ruto amechagua kutotii matakwa ya waandamanaji kwa kuachana na bajeti yake katika juhudi za kutuliza nchi.
Wengine katika serikali yake wanaweza kujiuliza kama msimamo huo anaweza kuendelea nao na unauacha vipi muswada wake wa fedha wenye utata.
Bw Ruto amedai kwamba msururu wa ushuru mpya ni muhimu ili kudhibiti deni la Kenya, kiasi kikubwa cha zaidi ya $80bn (£63bn), ambayo inagharimu nchi zaidi ya nusu ya mapato yake ya kila mwaka ya ushuru kwa huduma.
Kenya ilipata marekebisho ya ahadi zake za deni la kimataifa mapema mwaka huu – jambo ambalo lilisukuma mara moja kuongezeka kwa thamani ya sarafu yake.
Huku akionekana kuwa mmoja wa viongozi wakuu barani Afrika, aliyerejea hivi karibuni kutoka kwenye ziara ya kiserikali katika Ikulu ya White House, Bw Ruto anaelewa umuhimu wa uchumi wa taifa lake wa kuepuka kushindwa kulipa madeni yake.
Kwa wale wa serikali yake hesabu ilikuwa kwamba kudhibiti fedha za serikali kwa kuongeza mzigo wa kodi ilikuwa afadhali kukata huduma za umma.
Muswada huo, unaotarajiwa kuwa sheria Jumatatu ijayo, awali ulizua kodi nyingi mpya au zilizoongezwa kwa kila kitu kutoka kwa umiliki wa gari na miamala ya kifedha hadi taulo za kike.
Kodi kadhaa zenye utata tayari zimeondolewa kufuatia mashauriano na umma.
Lakini utata kuhusu bajeti hiyo unafuatia hatua nyingine za kuongeza mapato zilizoanzishwa na Bw Ruto, zikiwemo ongezeko la ushuru kwa huduma za afya na nyumba za bei ya chini.
Na kwa wale walio mitaani, kuna suluhisho la tatu linalopatikana kwa serikali zaidi ya kukata huduma au kuongeza kodi.
Wengi wanalaumu matatizo ya kifedha ya nchi kutokana na ufisadi, huku walipa kodi wakihofia kulipa zaidi huku kukiwa na ukosefu wa imani kuhusu uwazi wa serikali.
Kwa Bw.Ruto labda ni vivuli vya wakati uliopita vinavyofanya wadhifa wake wa sasa kuwa mgumu sana.
Anaweza kuwa rais mpya, na kwa kuzingatia nishati ya kijani na teknolojia bila shaka ana mawazo mapya kuhusu anakotaka kuipeleka Kenya.
Lakini kwa wengi mitaani, rekodi ya Bw Ruto kama kiongozi mkuu serikalini kwa muda uliokumbwa na ufisadi inamaanisha ni vigumu kumuamini.
Matukio ya jana jijini Nairobi yanamuacha Bw Ruto akionekana kubanwa vikali.
Huku akikabiliwa na shutuma kwa kile Wakenya wengi wanaona kama hatua kali dhidi ya maandamano mitaani, amelaumu moja kwa moja hatua ya maandamano hayo kutodhibitiwa.
Lakini wachache kati ya waliojitokeza kupaza sauti zao jijini Nairobi na kote nchini wanaonesha dalili zote za kutokata tamaa.
Bw Ruto alipohutubia taifa katika hotuba yake ya kuapishwa mwaka jana, alizungumza moja kwa moja na vijana wanaofanya siasa nchini.
“Safari yangu ya kisiasa,” aliwaambia, “vivyo hivyo ilianza kama mfanyakazi mchanga wa kujitolea, ambaye ametoka chuo kikuu.”
“Uzoefu wako na masomo uliyojifunza yanapaswa kuunda msingi wa safari yako ya uongozi.”
Sasa ni makabiliano na vuguvugu linaloongozwa na vijana ambalo linaleta kile ambacho wengi wanakichukulia kuwa changamoto kubwa zaidi kwa mamlaka nchini Kenya tangu uhuru wa nchi hiyo mwaka wa 1963.
Siku zijazo kwa Bw Ruto zitakuwa muhimu, huku mzozo ukiendelea kati ya serikali yake na watu wake walio wengi.