Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Kijiji cha Bima kimezinduliwa rasmi leo, Juni 28, 2024, katika Maonesho ya 48 ya Sabasaba yanayofanyika Dar es Salaam. Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) na wadau wake wamekusanyika katika tukio hili muhimu kuashiria umoja wao katika sekta ya bima, wakilenga kuboresha huduma za bima kwa Watanzania na kuhakikisha soko la bima linakuwa endelevu.