106 views 2 mins 0 comments

JOKATE AWATAKA VIJANA KWA WINGI KAMPENI MAALUM KUWAHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

In KITAIFA
July 04, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Katibu Mkuu UVCCM (MNEC) Jokate Mwigelo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika uwanja mkapa (Lupaso)  jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni maalum ambayo imelenga kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Wito huo ameutoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa kampeni hiyo itazinduliwa Julai 6, mwaka huu ambapo zoezi rasmi litafanyika mkoani Kigoma lengo ni kuhakikisha vijana wote wanashiriki kikamilifu katika zoezi la kujindisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Amesema kuwa, uzinduzi wa kampeni hiyo umelenga  kujadili fursa mbalimbali zilizotengenezwa kwa vijana na Serikali ya awamu ya sita ya chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluh hasani.

Aidha,amesema kuwa pia itakua ni fursa kwao wao umoja wa vijana wa Uvccm na vijana wote wa Tanzania kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali ya maendeleo hususani katika kujiandisha katika daftari la mpiga kura. 

Ameongeza kuwa, zoezi rasmi  la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litaanza Julai 20 mwaka huu, hivyo ni fursa pia kwa vijana kugombea nafasi za uchaguzi katika Serikali za Mitaa pia wanaomba vijana wajiandikishe katika daftari la makazi.

Aidha, kampeni hiyo ya uzinduzi huo utaongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Balozi Dkt Emanuel Nchimbi pamoja na Mwenyekiti wa Uvccm Taifa comred Moh’d Ali Kawaida na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa na Makamo Mwenyekiti Rehema Somba  pamoja na wenyeviti wa chama na jumuiya wa mikoa 32 na wao watashiriki kikamilifu katika uzinduzi wa kampeni hiyo.

“CCM tunafahamu madhumuni ya kuanzishwa kwa chama hiki ni kuleta mageuzi makubwa sana ya kimaendeleo kiuchumi kijamii kisiasa na kiutamaduni ambapo tangu kuanzishwa kwake vijana tumekua mstari wa mbele na wameaminiwa kushika hatamu katika majukumu mbalimbali ili kuhakikisha maono ya chama cha Mapinduzi yanatimia”amesema Mnec Jokate .

Ameongeza”Niendelee kuwahakikishia vijana wote, CCM inatambua tunayonguvu ya kuibua mawazo mapya katika ujuzi na ubunifu katika kusukuma gurudumu la maendeleo, hivyo basi nawalika watanzania wote hususani vijana kwenye uzinduzi wa kampeni hii kushiriki kikamilifu na ufanisi wa hali ya juu mara baada ya uzinduzi wake”.

/ Published posts: 1414

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram