-Asikikiliza maoni na ushauri katoka pande zote mbili wafanya biashara wakubwa na machinga
-Aelekeza kuundwa kamati ambayo itaongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 06,2024 amekutana na kufanya kikao na viongozi wa wafanyabiashara wakubwa na machinga wa kariakoo katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazimmoja Ilala.
Kikao hicho kiliwajumuhisha wakuu wa wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya wakurugenzi na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila.
RC Chalamila kupitia kikao hicho alipata wasaa wa kuwasikiliza vongozi wa Machinga na viongozi wa wafanyabiashara juu ya namna bora ya kuondoa migongano ya kibiashara kati ya wafanyabiashara wakubwa wa kariakoo na machinga ambao wamekuwa wakilalamikiwa kufanya biashara mbele ya maduka na kufunga baadhi ya mitaa ya kariakoo.
Aidha baada ya kuwasikiliza kwa makini RC chalamila ameelekeza kuundwa kwa kamati ambayo itakuja na majibu au suluhu ya malalamiko katika pande zote mbili, upande wa machinga na wafanyabiashara wakubwa,kamati hiyo itaongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa pamoja na wajumbe wengine watakaochaguliwa ambapo ametaka kamati kufanya kazi kwa haraka iwezekanavyo.
Sanjari na hilo RC Chalamila amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala na wataalamu wake mapema iwekanavyo kuja na proposal ya ushauri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan juu ya namna bora ya kuwapanga machinga, pia machinga wenyewe waketi waanishe ni kipi wangependa serikali iwasaidie ili kumaliza migogoro yao.
Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa wafanyabiashara hao kutanguliza upendo nyakati zote kwa kuwa makundi yote mawili wahitajiana pia kuendelea kuilinda amani katika Mkoa huo kwa nguvu zote.