Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb) ameihakikishia sekta binafsi hususani Wafanyabiashara na
Wawekezaji wa Viwanda kuwa watapata ushirikiano mkubwa katika kutatua changamoto mbalimbali za kibiashara ili kuhakikisha wanafanya biashara kwa chini ya uongozi wake.
Ameyasem hayo Julai 5, 2024, alipokuwa akizungumza na baadhi ya Taasisi zilizochini ya Wizara yake zinazofanya kazi kwa ushirikano kati ya Tanzania Bara na visiwani zinazohusika na masuala ya biashara mara baada ya hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu ndogo Tunguu, Zanzibar,
Aidha Dkt Jafo ametiwa wito kwa Wizara za Kisekta na sekta binafsi Bara na Visiwani kushirikiana kwa karibu na Wizara yake ili kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara na kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan inayo
Vilevile, ameahidi kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali wakabili wafanyabiasha, wamiliki wa viwanda na sekta binafsi kwa ujumla inayoajiri watu wengi zaidi nchini ili kuongeza ajira, pato la taifa na kujenga uchumi imara na shindani wa viwanda.
Dkt. Jaffo pia amesema akiwa pamoja na wataalamu wake ataendelea kukutana na wafanyabiashara mbalimbali kupitia mabaraza ya biashara katika mikoa yote nchini kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kujipanga jinsi ya kuzitatua ili kuhakikisha sekta ya viwanda na biashara inakua na kuongeza ajira, Pato la Taifa na kujenga uchumi imara na shindani.
Aidha, ameagiza kila Mtumishi wa wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake kutimiza wajibu wake kwa weledi na ufanisi ili kuhakikisha Wizara hiyo inafikia matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kukuza Sekta ya Viwanda na Biashara.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamis wamemuahidi Waziri Jaffo kuwa wako tayari kushirikiana naye katika kutekekeza majukumu na maelekezo yote yaliyotolewa kwa wizara hizo ili kufikia malengo tarajiwa