294 views 2 mins 0 comments

WAZIRI JAFO AWAOMBA WAWEKEZAJI WAJITOKEZE KWA WINGI KUWEKEZA KATIKA NCHI YA TANZANIA

In BIASHARA, KITAIFA
July 07, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Waziri wa viwanda na biashara Suleiman jafo Leo ametembelea Katika maonyesho 48 ya Kimataifa ya Sabasaba ambayo yanakuwa Kwa kila mwaka wa mwezi wa Saba na watu wa mataifa wote wanakuwa hapo Kwa ajili ya kutangaza biashara zao

Waziri wa viwanda na biashara Suleiman jafo Amesema Katika maonesho haya nchi mbalimbali zinashiriki hasa kukumbuka siku zao za mataifa Yao Leo hii wamekuwa na nchi ya china



“Kama unavyofahamu sisi na nchi ya china tunamahusiano ya Muda mrefu Zaidi ya miaka 60, Mahusiano haya yameleta.faida kubwa sana Katika nchi zetu hizi mbili Jambo la kwanza Mahusiano Katika upande wa kiuchumi munafahamu.jinsi Gani tunavyosafirisha bidhaa,Zaidi ya Dola za kimarekani Bilioni 3.3 tunasafirisha.na kingine ni bidhaa kutoka china Zaidi ya thamani bilioni 3.5 munaona hapo tunamahusiano makubwa sana”Amesema jafo



Jafo Amesema swala zima la uwekezaji miradi mbalimbali na viwanda mbalimbali Kuna viwanda vizuri sana Katika china na nchi yetu ambavyo Katika namna nyingine vinatoa ajira Katika wananchi wetu na hata kwenye ujenzi wa miundombinu, Mahusiano yetu yamesaidia hata ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchi ya china Kupitia Kwa Kampuni yake wanaweza kufanya kazi kubwa ya ukandarasi Katika nchi yetu



Aidha Ameongeza kuwa Leo kulikuwa na jambo kubwa Katika makampuni Zaidi ya mia Moja yameweza kushiriki Katika maonesho haya,na makampuni yote yametoka china

“Tunavutia wamekezaji Katika nchi yetu binafsi kama serikali ya Rais Samia imeamua na kuhakikisha kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha wawekezaji wanapata fursa ya kuwekeza vizuri Katika nchi yetu”Amesema Jafo



Amebainisha kuwa wataendelea kushirikiana Katika ofisi yao ya viwanda na Biashara ikihusika Katika miradi ya viwanda wanawakaribisha Kwa wale ambao wanaitaji kuwekeza hasa kutoka china na hata nchi mbalimbali waweze kufanya jambo hilo maana itasaidia sana Katika ujenzi wa uchumi Katika nchi yetu lakini hususani Katika upatikanaji wa ajira Kwa Vijana wetu” kama munavyofahamu Sasa hivi Vijana wetu wanamalizia vyuo vikuu na serikali haiwezi kuajili Vijana wote”Amebainisha Jafo

/ Published posts: 1934

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram