Na Mwandishi wetu WAMACHINGA
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt Selemani Jafo aliwasisitiza wafanyakazi wa wizara na taasisi zilizochini yake kufunga mkanda kuhakikisha sekta ya viwanda na biashara zinapiga hatua.
Dkt. Jafo aliyasema hayo Julai 08, 2024 wakati akiongea na Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Balozi John Stephen Simbachawene mara alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo Julai 08,2024 Mtumba Dodoma.
Aidha, aliwasisitiza Watumishi hao kuacha kufanyakazi kwa mazoea, kuzingatia muda na kufanya kazi kwa weledi na kwa kushirikiana
“Nimekuja tufanyekazi pamoja ili tumsaidie Rais, naomba ushirikiano kwani wizara inamambo mengi na tuna kazi kubwa ya kufanya hasa katika masuala ya viwanda vinavyoajili watu wengi zaidi,”Alisema Dkt Jafo
Kwa upande wa sekta ya biashara, Dkt. Jafo alisema wanapaswa kuweka kipaumbele sekta hiyo kwa kuhakikisha wanaweka mazingira bora na wezeshi ya ufanyaji biashara.
Alisema wakifanya hivyo wataondoa tishio ya migomo kama iliyojitokeza hivi karibuni ya wafanyabishara kutishia kufunga biashara katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Dodoma.
Awali, akimkaribisha, Naibu Katibu Mkuu, Balozi John Simbachawene alisema wizara inajukumu la kuleta maendeleo jumuishi na endelevu, kuchocheza maendeleo ya sekta zilizochini yake na kulifikisha taifa katika kiwango cha uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo 2025.
Alisema kwa sasa iko katika mchakato wa kufanyia marejeo sera, sheria na mikakati mbambali ili ziendane na wakati wa sasa katika sekta za viwanda na biashara na kumuahisi kumpa ushirikiano.