Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Injinia Felchesmi Mramba amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),
Akiwa kwenye banda EWURA ndani ya Maonyesho ya 48 Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) leo tarehe 9Julai 2024 Mramba amesema bei ya huduma husika ipo chini na wanatoa huduma ya umeme
Akitolea mfano bei ya Umeme kwahivi sasa nchini kwetu ipo chini ukilinganisha na Mataifa mengine ya Afrika Mengine ya Afrika Mashariki
“Ukiangalia bei ya Umeme wetu ipo chini sana na Waandishi wa habari mnajua sababu ninyi mnaweza kufatilia kwenye Website(TOVUTI) za nchi Mbalimbali” alisema katibu mkuu Mramba.
Aliongeza kuwa Ubora wa Umeme kwa siku za hivi Karibuni zimeimarika kule kukatikakatika (MGAO) kwa sasa hakuna,kwa hiyo tunaendelea kuboresha na niwajibu wa EWURA kusimamia.
Bwana Mramba alisema kwa upande wa Gesi asilia EWURA anasaidia sana,anatoa Leseni hasa kwa wale wanaojenga vituo vya (CNG),lakini pia EWURA inahakikisha ile huduma inayotolewa inakidhi mahitaji ya Jamii.
Aliongeza kuwa Wizara ya Nishati itahakikisha kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Ewura Dkt James Andilile amesema wameingia mkataba na TANESCO kwalengo la kusimamia utendaji kazi wao ili kuboresha utendaji na upatikanaji wa Umeme na kwa sasa Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Nishati ili kuhakikisha sekta hiyo inaimatika
Kwaupande wa Bei ya Mafuta Beana Ndilile amewataka wale wote wanaohitaji kuwekeza kwenye sekta ya gesi kujitokeza kwani gesi inapatikana hapa nchini ili kuwahudumia wananchi