Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Mwenyekiti wa Wasanii na Muigizaji Steve Nyerere Wamemuomba Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kuwa kipaumbele Chao Cha kwanza ni Elimu Kwa wasanii
Amesema kuwa Kuna watu wanaitajika kupewa elimu ni Director,Camera Man, Producer na Editor
Hayo Ameyasema Leo 11,Julai 2024 Mwenyekiti wa Wasanii na Muigizaji Steve Nyerere wakati wakitoa taarifa kuhusiana walivyoenda Korea Kwa kujifunza maswala ya uigizaji Kwa msaada wa Rais Samia
“Director kwanza inabidi kuwa na maono ya mbali,lazima tutafute Madirector wa hapa kwetu wenye ubora,Nidhamu,wenye uthubutu wakapate elimu”Amesema Nyerere
Steve Ameeleza kuwa Elimu itawasaidia kutengeneza vitu vizuri, Camera Man, Producer na Editor hawa watu bila kupewa elimu tutakuwa tunapoteza Muda kwani Hawa watu inabidi wapewe vipaumbele
“Tumeenda Korea na katika safari ile tumejifunza vitu ambavyo vingine hata tulikuwa haruvijui,kimoja wapo ambacho tulianza kujifunza mtu mmoja kumiliki kazi 14 kwenye tamthilia yake”
“Wewe ndo tunakuwa director,wewe ndo unakuwa camera man,wewe ndo script Late,wewe ndo mtafuta vision ya kushutia wewe ndo kila kitu na unapewa fedha ya kuandaa tamthilia yako wezetu kule wanajigawa kama mcheza filamu anabaki kuwa mcheza filamu zote hizo ndo ajira ndomana wezetu wanaingiza mapato makubwa” Ameongeza Nyerere