137 views 2 secs 0 comments

DKT BITEKO CHAGUENI VIONGOZI WA MAENDELEO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

In KITAIFA
July 22, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Awataka kujindikisha na kujiandaa kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kuchagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwenye uchaguzi mwaka huu ambao watakuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo na kutatua changamoto zao kwa haraka.



Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara kijiji cha Lyambamgongo wilaya ya Bukombe mkoani Geita.



โ€œMuda utakapofika tuwe tayari kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ili tuweze kuchagua viongozi wazuri wenye sifa za kuchaguliwa ambao watasaidia kuleta maendeleo, tunataka jimbo la Bukombe libadilike kwa kuwa na watu wenye maono au mawazo mazuri yatakayosaidia utatuzi wa changamoto zinazotukabiliโ€, amefafanua na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram