Na Anton Kiteteri WAMACHINGA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Daktari Dotto Biteko ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na kuheshimiana na viongozi wao ili kuwapa nafasi ya katimiza wajibu wao wa kuwaletea maendeleo badala ya kukwamishana.
Dk. Biteko ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msangila,kata ya Runzewe magharibi,wilaya ya Bukombe,mkoa wa Geita.
Mheshimiwa Biteko amefafanua kuwa dhamira ya rais Samia Suluhu Hassan ni kuwaona Watanzania wanapata maendeleo katika nyanja za elimu,afya, barabara, umeme na miundo mbinu ya mawasiliano na teknolojia,na ndio sababu katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameleta maendeleo kwa kasi kubwa.
“Sisi wasaidizi wake anatuagiza muda wote tukawasikilize kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati na niko hapa kuwambia kuwa mheshimiwa rais Samia anawapenda na amekusudia kuwapa maendeleo”, Alifafanua Dk.Biteko.
“Hapo mwanzo tulikuwa na shida ya umeme na ulikuwa ukikatika mara kwa mara kutokana na mahitaji kuwa makubwa na wakati huo huo umeme ulikuwa mchache na kutokana na mheshimiwa rais kusimamia vyema sekta hii kwa sasa tatizo hilo halipo na tunaendelea kuimarisha miundo mbinu ya umeme”, Alisisitiza Mh.Biteko.
Dk Biteko amesisitiza uvumilivu kwa diwani wa kata hiyo,Kwa kumwambia kuwa ana wajibu wa kuwaletea maendeleo wananchi bila kujali nani anampenda na nani hampendi bali atimize wajibu wake kwa kushirikiana na wale walioamua kumuunga mkono.
“Duniani tumeumbwa makundi ya watu watatu,wapo watakao kupenda,wapo watakao kuchukia na wapo ambao hawajui wakupende ama wakuchukie,wewe shughulika na wanao kupenda na wale ambao hawajaumua kupenda au kukuchukia”, Alisisitiza Dk.Biteko.