260 views 3 mins 0 comments

SGR YALETA TASWIRA MPYA USAFIRISHAJI, SAFARI DAR ES SALAAM NA DODOMA KUANZA RASMI

In KITAIFA
July 26, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Shirika  la reli Tanzania (TRC) Leo hii imeanza Kutoa huduma za safari kutoka dar es salaam  kuelekea mjini dodoma ambapo shirika hilo limesema kuwa utekelezaji huo umetokana na juhudi za Mhe Rais Samia suluhu Hassan Ambapo alitoa maelekezo kuwa ifikapo julai mwaka huu 2024 TRC iwe imeshatekeleza mradi wake wa kutoa huduma ya usafiri Kwa wananchi Kwa kuelekea mkoani Dodoma.


Ameyasema hayo Leo Tarehe 25,Julai 2024  Mkurugenzi wa shirika la Reli nchini Tanzania Masanja Kadogosa  amesema kuwa  kutoka Dar es salaam kuelekea mkoani Dodoma usafiri huo unaenda kurahisisha  baadhi ya wasafiri  ambao wanatoka sehemu mbalimbali  kupitia maeneo ya dar esalaam kuelekea mkoani humo.


Amesema kama shirika wanamshukuru Mungu kwa kukamilisha jambo hilo Kwa wananchi ambao walikuwa wanalisubiria Kwa shauku kubwa.


“Tuna  viongozi. Mbalimbali   kwenye treni hii ya leo ambayo inaanza rasmi safari za Dar es salaam kuelekea dodoma pia siku za hivi karibuni tutatoa taarifa rasmi ya uzinduzi wa treni hiyo  huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Dkt samia suluhu hassani”. Amesema Kadogosa


Aidha  Mkurugenzi. Kadogosa. Aliongeza  kuwa treni hii inaweza Kubeba mabehewa zaidi ya 14 hadi 20 huku mabehewa hayo yakiwa yamebeba abiria Takribani ya 900. Vilevile baadhi ya Abiria wamekosa tiketi za kuondoka Dodoma hivyo tumeona  muamko Mkubwa wa wananchi na kuweza kufurahia usafiri huo wa haraka ambao unatumia muda mchache wa kutoka. ” Amesema  mkurugenzi  kadogosa”.

Kadogosa Ameongeza kuwa Treni Zetu  zipo aina mbili tofauti. Ambazo ni daraja la juu na kawaida kupitia bei elekezi. Ya Mamlaka ya usafiri wa Ardhini ( Latra). Kiwango cha fedha cha kawaida ni elfu thelathini na moja kutoka dar esalaam kuelekea dodoma huku nauli za Kutoka mkoani dar es salaam mpaka Morogoro ni 13000.


Kwa. Upande. Wake  Abiria kutoka. Dar es salaam kuelekea mkoani dodoma. Rose mchau. Amesema kuwa  leo nina furaha kubwa  ya kupanda. Treni.hii ya mwendokasi  kwani wameturahisishia katika  kutumia muda mchache wa safari ikiwa na tofauti  na Magari ya kawaida.


Vilevile  Rose ameongeza. Kuwa. Mimi ni mkazi wa dodoma hivyo nilivoona treni hii imekamilika. Pia nawashauri  wananchi wote wafike kupanda treni hii kwani ni nzuri. Pia Ina mazingira. Wezeshi kwa watu wa rika zote na mahitaji maalumu pia ni matumaini yangu kuwa  katika safari yetu hii tutafika salama

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram