Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Kiongozi Mstaafu wa ACT Wazalendo Ndg. Zitto Kabwe amesema Serikali imetengeneza uchumi dumavu usiozalisha ajira na kuwatelekeza vijana.
Akizungumza na wananchi akiwa Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma jana Julai 24, 2024 amesema tatizo la ajira linatishia utulivu na kusababisha vijana wengi wasio na ajira kuwa tegemezi.
“CCM isifikirie kuwa Gen Z haiwezi kuibuka Tanzania, vijana wasiokuwa na ajira watachoka na kujipanga kudai haki zao. Kati ya nguvukazi ya watu Milioni 33.2 ni watu wachache tu (milioni 3) ndio wameajiriwa rasmi katika sekta za umma.”
Ndg. Zitto amesema tatizo linakuwa kubwa kila siku chini ya CCM hadi tumefikia wahitimu wa vyuo vikuu wanaenda kuwa wamachinga, madereva wa bodaboda. Ni kupoteza nguvukazi ya taifa kuwaingiza wataalamu wetu katika kazi wasizozisomea.