Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Leo tarehe 27 Julai 2024, Watumishi wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake wameshiriki katika michezo mbalimbaliย katika Bonanza la Nishati Jijini Dodoma likibebwa na Kaulimbiu Shiriki Michezo Imarisha Afya.
Mgeni rasmi katika Bonanza hilo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu , Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe.Judith Kapinga na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule.
Baadhi ya Michezo inayofanyika kwenye Bonanza hilo ni Kupokezana vijiti wanaume, Kupokezana Vijiti Wanawake, Rede, Karata, Riadha, Kukimbia na yai,ย Kukimbia ndani ya gunia, Kukimbia na maji kwenye glasi, Kupenya ndani ya pipa, Mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Bao na Karata.