Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba TMDA imebaini kuwepo Kwa taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii Kuhusu uwepo wa dawa aina ya paracetamol ambayo imeandikwa P 500 na kudaiwa kubabua ngozi
Ameyasema hayo mkurugenzi wa Dawa na vifaa tiba TMDA Adam Fimbo Amesema Dawa iyo inayodaiwa kuwa ni “paracetamol mpya nyeupe sana na inayong’aa” madaktari wanashauri kuwa ina virusi vya ‘MACHUPO’ inayochukuliwa kuwa Moja ya virusi hatari Zaidi ulimwenguni, na kiwango Cha juu Cha kifo.
Fimbo Anafafanua kuwa Mtoa Taarifa anaitaka jamii kuisambaza taarifa hii Kwa kila mtu aliyoko Katika orodha yake ya mawasiliano Ili kuokoa maisha, anamaliza Kwa kusema ,”nimefanya Kwa sehemu yangu, Sasa ni zamu yako,kumbuka kwamba mungu huwasaidia wale wanaosaidia wengine, “sambaza Kama ilivyopokelewa”.
Aidha Amebainisha kuwa Taarifa hiyo imekuwa ikijirudia Rudi mara Kwa mara na TMDA imekuwa ikitolea ufafanuzi ikiwemo taarifa ya mnamo tarehe 10 Mei 2023 juu ya dawa ya aina P 500@(PARACETAMOL) ya Apex Laboratories private limited, Tamil Nadu, India inayodaiwa kuwa na virusi hivyo.
Fimbo Anafafanua kuwa TMDA inapenda kuufahamisha umma Kwa mara nyingine tena kwamba hakuna virusi vinavyojulikana Kwa jina la machupo,Aidha virusi vya aina yoyote haviwezi.kuishi kwenye vidonge.
“Dawa zenye kiambata hai Cha paracetamol inayotumika kutibu homa na maumivu zilizopo Katika soko nchini Kwa majina mbalimbali ya kibiashara zimesajiliwa baada ya kuthibitishwa kuwa zinakidhi vigezo vya usalama,ubora na ufanisi unaotakiwa na hivyo ni salama Kwa matumizi yaliyoainishwa”.Amefafanua Fimbo
Aidha TMDA inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa inaendelea kutimiza wajibu wake wa kulinda Afya ya jamii Kwa kuhakikisha kuwa Bidhaa tiba zinazotumika nchini ni zile zenye kukidhi matakwa ya ubora,usalama na ufanisi.
Vile vile mamlaka inapenda kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kupata ufafanuzi kutoka kwenye mamlaka husika kabla ya kusambaza taarifa zinazoweza kuleta taharuki katika jamii.