Na Anton Kiteteri
Chama Cha ANC kimemfukuza uanachama rais wa zamani wa Africa Kusini Jacob Zuma.Uamuzi huo ambao haujatangazwa rasmi, ulichukuliwa baada ya kesi za kinidhamu kuanzishwa mwezi huu dhidi ya kiongozi huyo wa zamani ambaye bado ana umaarufu na ushawishi mkubwa nchini humo.
“Mwanachama aliyeshtakiwa amefukuzwa katika chama cha ANC,” umesema waraka uliovuja, ambao umeonwa pia na shirika la habari la AFP ambao ni wa tarehe 29 Julai.Hata hivyo aliyeshtakiwa ana haki ya kukata rufaa kwa kamati ya kitaifa ya nidhamu ya rufaa ndani ya siku 21.
Chama cha African National Congress (ANC) kilimsimamisha kiongozi huyo wa zamani aliyokumbwa na kashfa mwezi Januari, mwezi mmoja baada ya kukiunga mkono chama kipya cha uMkhonto weSizwe (MK).MK kilipunguza kura za ANC katika uchaguzi wa tarehe 29 Mei, na kuchukua nafasi ya tatu kwa asilimia 14.5 za kura ya kuwa zote.
Zuma hivi sasa anaongoza chama hicho, ambacho kina wabunge 58 katika bunge la taifa lenye viti 400.ANC kilipata asilimia 40 ya kura ya zote katika uchaguzi wa Mei 29, zikiwa ni kura chache sana tangu kiingie maradakani miongo mitatu iliyopita kuchukua nafasi ya serikali ya ubaguzi wa rangi.
Mbali na rufaa iliyofanikiwa dhidi ya uamuzi huo, uanachama wa Zuma ndani ya ANC unaweza kufutwa kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vyombo.Zuma alijiunga na ANC kupitia tawi la vijana la chama hicho akiwa na umri wa miaka 15 mwaka 1959.