173 views 8 secs 0 comments

WANANCHI 1404 WAITWA MAUNGANISHO YA MAJI SAFI DAWASA

In KITAIFA
July 29, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na zoezi la kugawa vifaa vya maunganisho mapya ya huduma ya Majisafi kwa wateja walioomba huduma ndani ya eneo la kihuduma la DAWASA ambayo ni Mikoa ya Pwani na Dar es salaam.

Zoezi hilo limeendelea katika Mikoa ya kihuduma DAWASA Kinyerezi, DAWASA Mapinga, DAWASA Kawe, DAWASA Bagamoyo, DAWASA Mabwepande, DAWASA Tegeta na DAWASA Makongo na jumla ya Wananchi 1404 wameitikia zoezi hilo.

Sambamba na zoezi hilo, Mamlaka imetoa elimu mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu ya utunzaji wa miundombinu, matumizi sahihi ya Maji, njia rasmi za mawasiliano na malipo ya Ankara pamoja na taarifa nyingine muhimu zitolewazo na DAWASA.

Zoezi hili ni muendelezo wa juhudi za DAWASA za kusogeza huduma ya Majisafi kwa Wananchi wanaopatikana ndani ya eneo lake la kihuduma.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram