135 views 2 mins 0 comments

DAR-SGR MIKUMI TOUR KWA AJILI YA WALIMU

In KITAIFA
July 30, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA t

-Zaidi ya walimu 1000 kupanda Treni ya ya Umeme SGR kwenda Hifadhi ya Taifa Mikumi-Morogoro

-Lengo ni kuunga mkono Juhudi za Mhe Rais Dkt Samia kufuatiaย 
uwekezaji mkubwa alioufanya katika usafiri wa reli ya SGR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 30,2024 akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala boma ametoa taarifa kwa umma juu ya uzinduzi wa Treni ya SGR ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Dodoma Agosti 01,2024

Akiongea mbele ya waandishi wa habari RC Chalamila amesema ofisi yake imeandaa Safari SGR Mikumi Tour kwa walimu wa Mkoa huo, ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti 02,2024 siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kufanya uzinduzi wa SGR Mkoani Dodoma

Aidha RC Chalamila amesema program hiyo inaanza kufanyika kwa kundi la walimu Zaidi ya 1000 na itaendelea kufanyika kwa makundi mengine kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia kutokana na utekelezaji wa kishujaa wa mradi mkubwa wa SGR ambao unakwenda kurahisisha na kuweka rekodi ya kihistoria na mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri wa reli ndani ya nchi na nje ya nchi hususani barani Afrika.

RC Chalamila ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za kishujaa zinazofanywa na Mhe Rais katika Nyanja mbalimbali hapa nchini ili kumtia moyo ambapo amesema katika tukio la kukata utepe katika mradi wa SGR akiwa Dar es salaam wanachi wajitokeze kwa wingi.

Mwisho Safari ya SGR Mikumi TOUR kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni ya Siku 2 Siku ya kwenda Ijumaa Agosti 02,2024 na Siku ya Kurudi Jumamosi Agosti 03,2024 ambapo msafara utaanzia Stesheni kuu ya SGR-DSM.

/ Published posts: 1440

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram