Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA ZANZIBAR
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amekagua banda la Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika tamasha la KIZIMKAZI linaloendelea Visiwani Zanzibar.
Wizara ya Nishati inashiriki katika tamasha hilo kupitia Maonesho ambayo Wizara inatoa huduma moja kwa moja kwa wananchi kwa kushirikiana na Taasisi zake pamoja na kutoa elimu ya Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa mwaka 2024-2034.