
Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM
Waziri wa Viwanda na Biashara pia ni Mbunge wa Jimbo la kisarawe mkoani pwani Mh.Suleiman Jafo, amewataka Wananchi wa Jimbo la kisarawe na watanzania kwa ujumla kujitokeza katika kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura Ili kumchagua kiongozi imara atakaewaletea maendeleo Katika majimboni kwao
Ameyasema hayo Tarehe 31 Agosti 2024 Waziri wa Viwanda na Biashara pia ni Mbunge wa Jimbo la kisarawe Mhe Suleiman Jafo Akiwa Katika kwenye kilele cha Tamasha maalum la Sanaa mtaa kwa mtaa lililofanyika Jana
Mhe Jafo Amesema lengo la kufanya Tamasha hilo la Sanaa mtaa kwa mtaa ni kuwahamasisha wananchi na watanzania kujitokeza Kwa wingi kujiandikisha Katika Daftari la wapiga kura Kwa ajili ya kumtafuta kiongozi unaemtaka na anaweza kuendesha sera ya nchi.
“wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Vitongoji na mitaa Nchini unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu ni haki ya kila mwananchi kujitokeza na kuhakikisha anajiandikisha kwenye Daftari Hilo ili Kujiandaa kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi huo”.Amesema Jafo
Aidha Jafo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara ametumia fursa hiyo kumpongea RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake katika kuwaletea maendeleo Wananchi Jimbo la kisarawe ikiwemo Maji, Elimu, afya pamoja na Umeme.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya kisarawe Mhe Petro Magoti amesema kisarawe ya wakati huu imepiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya muongozo WA Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkondo mh Rais Katika harakati za kuhakikisha anipeleka mbele nchi katika nyanja mbalimbali.
Aidha Magoti ametumia hadhara hiyo kuwaalika wadau mbalimbali kushiriki kwenye TAMASHA kubwa la utalii wa ndani hususani kwenye wilaya ya kisarawe lijulikanalo kama KULA BATA MSITUNI 2024.
Tamsha ambalo limepangwa kufanyika kuanzia Septemba 22 2024 kwenye msitu wa Kazimzumbwi, Tamsha ambalo linalenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya wilaya hiyo huku mataifa Zaidi ya sita yakitaraji kushiriki Tamsha Hilo.
Kwenye Tamasha hilo limeudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo waziri wa viwanda na biashara Suleiman Jafo, Mkuu wa Wilaya ya kisarawe Petro Magoti,Das na viongozi wengine.