251 views 3 mins 0 comments

MHANDISI SEFF ZAIDI YA MILIONI 46 ZIMESHATUMIKA KUREKEBISHA BARABARA ZA WILAYA

In KITAIFA
September 02, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

Serikali Kupitia wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imefanikiwa kuongeza mtandao wa Barabara za Wilaya kutoka kilomita 108,946,19 Hadi kilomita 144,429,77

Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff Ameyasema hayo Leo September 2,2024 jijini Dar es salaam Katika kikao kazi Cha wahariri na waandishi wa habari chini ya uratibu wa ofisi ya Msajili wa Hazina TR

Mhandisi Seff Amesema kuwa mtandao wa Barabara hizo zimegawanyika Katika makundi matatu ikiwemo za Lami, Changarawe, na Udongo



Amesema Hadi kufikia Juni,2024 barabara za Lami za Wilaya zilikuwa kilomita 3,337,66 sawa na Asilimia 2.31

Kati ya hizo Mhandisi Seff Amebainisha kuwa hali ya barabara hizo kilomita 2,743,81zipo Katika hali nzuri, kilomita 445,18 zipo Katika hali ya wastani huku kilomita 148,68 zikiwa Katika hali mbaya.

Kwa upande wa Barabara za Changarawe Mhandisi Seff Amesema kuwa ni jumla ya kilomita 42,059,17 sawa na Asilimia 29,12



Akizungumzia hali ya barabara hizo za Changarawe, Mhandisi Seff Amesema Kilomita 21,890,53 zipo Katika hali nzuri kilomita 15,792,23 zipo Katika hali ya wastani huku kilomita 4,426,41 zikiwa Katika hali mbaya.

Vilevile Kwa upande wa Barabara za Udongo Mhandisi Seff Amesema ni jumla ya kilomita 99,032,93 ni sawa na Asilimia 68,57



Amesema kati ya barabara hizo za Udongo kilomita 16,118,65 zipo Katika hali nzuri kilomita 34,739,20 zipo Katika hali ya wastani huku kilomita 48,175,09 zikiwa Katika hali mbaya.

Mhandisi Seff Amesema kutokana na mchanganuo huo barabara nzuri zinaunda jumla ya kilomita 40,752,98 sawa na Asilimia 28.22


  
Mhandisi Seff Amesema kuwa, bajeti ya matengenezo ya barabara imeongezeka Zaidi ya mara tatu kutoka shilingi bilioni kutoka wastani wa shilingi bilioni 275 miaka minne iliyopita na kufikia shilingi bilioni 850 kuanzia mwaka 2021/2022

Ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazoukabili mtandao wa Barabara hizo Nchini Mhandisi Seff Amesema wamejiwekea vipaumbele muhimu vinne Ili kusimamia ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao huo



Miongoni mwa vipaumbele hivyo,ni matengenezo ya miundombinu ya barabara Ili kulinda uwekezaji ambao tayari umeshafanyika Nchini,Kwa Kuendelea na matengenezo hata pale barabara na madaraja yanapokamilika Ili miundombinu hiyo iweze kudumu Kwa Muda mrefu Nchini.



Mhandisi amesema, Tanzania kwakushirikiana na Benki ya Dunia pamoja na Jumuiya ya Ulaya wanatekeleza mradi wa kujenga Barabara za Wilaya, ambapo Tayari Euro Milioni 46 zimekwisha tumika katika awamu tatu ambapo miradi hiyo bado inaendelea kujengwa

Aidha amesema katika Miradi inayojengwa kwa ushirikiano na World Bank

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram