Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Serikali ya Marekani (USG) yatoa huduma za VVU na chanjo kwa takribani vijana 10,000 wenye umri wa miaka 15-24 kupitia mpango wa Ndondo Cup Dar es Salaam.
Ndondo Cup ya mwaka huu imekuwa zaidi ya mashindano ya soka ya kienyeji; imegeuka kuwa mpango muhimu wa uhamasishaji wa afya ya umma, ikitoa huduma muhimu za VVU na chanjo kwa takribani vijana 10,000 wenye umri wa miaka 15-24.
Mabadiliko haya makubwa yametokana na juhudi za pamoja za Serikali ya Marekani kupitia USAID na PEPFAR, kwa kushirikiana na mradi wa Breakthrough ACTION, MDH, EPIC, Wizara ya Afya, na waandaaji wa Ndondo Cup. Waziri Nyoni, Mkurugenzi wa Mradi wa Breakthrough ACTION nchini Tanzania, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano:
“Mafanikio ya mpango huu yanaonyesha umuhimu wa ushirikiano katika kuboresha afya ya umma. Juhudi za Serikali ya Tanzania na washirika wa Serikali ya Marekani zilikuwa muhimu katika kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa huduma muhimu za afya kwa wanaume na vijana.”