Mazungumzo yanaendelea kati ya Chelsea na AEK Athens kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 21. (Mail)
Tottenham wamefanya mazungumzo ya kumnunua kiungo wa kati wa Marekani Johnny Cardoso, 22, kwa £21m kutoka Real Betis. (Telegraph – Subscription Required)
Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Naby Keita, 29, yuko kwenye mazungumzo na Istanbul Basaksehir kuhusu uwezekano wa kuhama kutoka Werder Bremen baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea kutokubaliana na masharti ya kuhamia Sunderland. (Guardian)
Chanzo BBC swahili