Winga wa zamani wa Manchester United Anthony Martial, 28, amepewa mkataba na AEK Athens ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo. Mfaransa huyo alikua mchezaji huru wakati kandarasi yake United ilipoisha mwezi Juni. (Sport24 via Sun).
Manchester United inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Juventus mwenye umri wa miaka 23 kutoka Colombia Juan Cabal. (Tutto Juve – In Italy), nje
Real Betis walitoa ofa kwa kiungo wa kati wa Manchester United na Denmark Christian Eriksen, 32, siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho (Fabrizio Romano)