Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Watanzania kunufaika na rasilimali zinazochimbwa katika maeneo yao kwa kutoa fursa mbalimbali ikiwemo ajira.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Septemba 10, 2024 mkoani Mtwara katika hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji wa eneo la ugunduzi wa gesi asilia katika Kitalu cha Ruvuma, eneo la Ntorya ambapo Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) pamoja na Kampuni za ARA Petroleum Limited na Ndovu Resources Ltd ni wabia.
“ Mhe. Rais alielekeza wananchi waliopo maeneo yenye rasilimali wanufaike kabla ya maeneo mengine, alitoa kibali cha mradi mkubwa wa gesi na tutajenga kiwanda cha kuzalisha gesi na kuboresha kituo za kuzalisha umeme Songa.” Amesema Dkt. Biteko.