120 views 0 secs 0 comments

BODI YA UTALII KUJA NA ONESHO LA SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO SITE

In KITAIFA
September 13, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya utalii Tanzania (TTB) inatarajia kuazimisha onesho la nane la SWAHILI INTERNATIONA TOURISM EXPO (S!TE) ambapo onesho hilo litafanyika kuanzia 11 mpaka 13 Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na waandishibwa habari mapema hii leo septemba 12,2024 Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya utalii nchini Ephraim Mafuru amesema onesho hilo ni muendelezo wa programu ya Tanzania Royal Tour iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kwa kusema kuwa  onyesho la S!TE 2024 lenye kauli mbiu inayoaema “Exprol Tanzania for a Life Time Investment and Seamless Tourism Experience”litafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam na kutoa rai kwa wadau wa Utalii hususan Mawakala wa utalii kushiriki katika onesho hilo.

/ Published posts: 1414

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram