150 views 6 secs 0 comments

MHE DEUS SANGU ATOA SALAMU ZA POLE KWA AFISA UGAVI MKOANI TABORA

In KITAIFA
September 22, 2024

Na Mwandishi wetu WAMACHINGA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu akiwa katika ziara ya kikazi  Wilayani  Uyui Mkoani Tabora amefika nyumbani kwa Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya  Uyui, Ashura Kangombe kwa ajili ya kutoa pole kufuatia msiba wa Mama yake  mzazi wa  Mtumishi huyo.

Mhe.Sangu amefika nyumbani hapo leo Jumamosi Septemba 21, 2024 akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wabunge wenyeji wa eneo hilo.

Akizungumza katika msiba huo, Mhe.Sangu amesema” Nimekuja Uyui kwa ajili ya kuzungumza na Watumishi wa  Wilaya ya Uyui nikiwa njiani nimeambiwa Bi.Asha Kangombe kafiwa, Mimi nikiwa  Mtumishi wa Watumishi nimekuja kumpa pole kwani asingepatwa na msiba huo angeshiriki kikao changu cha  kuzungumza na watumishi wa Uyui”

/ Published posts: 1440

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram