111 views 2 mins 0 comments

SAMIA ASIFU MCHANGO KIUCHUMI KWA SEKTA ISIYO RASMI

In BIASHARA, KITAIFA
October 05, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

RAIS Samia Suluhu Hassan amevunja ukimya na kutoa pongezi ya dhati kwa Sekta isiyo rasmi katika kuonesha jitihada kuchingia ukuaji wa uchumi kwa haraka kupitia shughuli mbalimbali za kujiajiri wenyewe.Takwimu zinaonesha kundi hilo lisilo rasmi linachangia asilimia 60 ya mapato yanayochangia kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Kauli hiyo aliitoa jana Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Tume ya Rais ya Kuthamini na Kushauri kuhusu Masuala ya Kodi, ambapo amewahimiza Watanzania kuwa mstari wa mbele katika kulipa kodi ili kufikia lengo la kujenga uchumi jumuishi, unaokua kwa kasi na unaoimarisha ustawi wa watu kwa kuboresha huduma za jamii na kupunguza umasikini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja.

“ Kwa kuzingatia mrejesho na maoni mbalimbali ya wananchi, wadau wa sekta binafsi na Wawekezaji wengine, Tume hii imeundwa kwa lengo la kufanya tathimini ya mfumo mzima wa kodi, kuimarisha zaidi mfumo huo na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kurahisisha usimamizi wa ukusanyaji wa kodi nchini.

AZIPONGEZA SEKTA BINAFSI

Mkuu huyo wa nchi alipongeza jitihada za Sekta binafsi kwa kuendelea kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi hasa wanapokuwa waaminifu katika ulipaji wa kodi, alibainisha kuwa licha ya uchumi wa nchi kukua kwa kasi, idadi ya watu kuongezeka na mahitaji ya huduma za kijamii na miundombinu kukua, bado asilimi 60 ya uchumi wa nchi unatokana na sekta isiyo rasmi,” alisema Rais Samia.

PONGEZI KWA TRA

Aidha, Rais Dkt. Samia ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA ) kwa kuiwezesha nchi kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa mwezi Septemba 2024. Alisema hatua hiyo imechangiwa na jitihada za Serikali kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato, kuijengea uwezo TRA, na kuimarisha mazingira ya kufanyia biashara nchini ikiwemo kufuta baadhi ya tozo na kuimarisha utendaji kwenye Idara, Wakala na Taasisi za Serikali.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram