45 views 0 secs 0 comments

NAIBU WAZIRI KAPINGA ASHIRIKI JUKWAA LA MAWAZIRI NCHINI AFRIKA KUSINI

In KITAIFA
October 08, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Lengo ni kutangaza fursa za uwekezaji kwenye Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala*

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga ameshiriki Jukwa la Mawaziri (Ministerial Symposium)ย  nchini Afrika Kusini ikiwa ni sehemuย  Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week) linalofanyika Jijini Cape Town.

Jukwaa hilo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio, Kamishina wa Petroli na Gesi Ndg. Goodluck Shirima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mha. Charles Sangweni.

Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.

Kongamano hilo litamalizika tarehe 10, Oktoba, 2024 nchini humo.

/ Published posts: 1435

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram