44 views 54 secs 0 comments

TAWA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA “SITE”

In KITAIFA
October 12, 2024



Utalii wa malikale wanadiwa

Na. Joyce Ndunguru, Dar es Salaam

Mamlaka ya Usimamizi wa   Wanyamapori Tanzania (TAWA) inashiriki maonesho ya Nane ya Kimataifa ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yaliyozinduliwa Leo Oktoba 11, 2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Maonesho haya ya kimataifa ya SITE yenye kauli mbiu ” Tembelea Tanzania kwa uwekezaji endelevu na utalii usiomithirika” inawakutanisha waoneshaji wa bidhaa na huduma za utalii takribani 120 kutoka ndani na nje ya nchi.

Ujumbe wa TAWA umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mej. Gen (Mstaafu) Hamis Semfuko akiambatana na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA Mabula Misungwi Nyanda.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa maonesho haya, Meja.Jen (Mstaafu) Semfuko amesema TAWA inatumia maonesho ya SITE kunadi mazao yake ya utalii ikiwemo utalii wa malikale unaofanyika katika  Hifadhi ya Urithi wa utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani pamoja na Kunduchi.

Sambamba na hilo,  TAWA inatumia maonesho haya ya kimataifa kutangaza bidhaa zake za Utalii wa picha  zinazopatikana katika Mapori ya Akiba ya Pande (Dar es Salaam), Wamimbiki (Pwani), Mpanga/Kipengere (Njombe na Mbeya), Kijereshi (Simiyu) sanjari na Utalii wa Uwindaji unaofanyika katika maeneo mengi yaliyo chini ya Usimamizi wa taasisi hii nchini.

Maonesho ya SITE, yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku tatu na yatafikiwa kikomo Oktoba 13, 2024.

/ Published posts: 1440

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram