30 views 2 mins 0 comments

DC BOMBOKO AIPONGEZA TAASISI YA YEMCO KUSAIDIA VIKUNDI VYA VIKOBA

In BIASHARA
November 01, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Mkuu  wa wilaya ya ubungo,Mh Hassan bomboko ameipongeza Taasisi ya Yemco kwa kusaidia vikundi vya vikoba vga akina mama mbalimbali nchini kufikia Malengo yao kiuchumi na KIJAMII.


Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka 8 wa Taasisi hiyo, uliofanyika Leo Oktoba 31 2024 jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 1000.

Bomboka amemshukuru YEMCO ambayo inayojihusisha na vikundi vya vikoba kwa ajili ya kuwania wanawake na wanaume ambao wamekuwa Wakitoa mikopo kwa kusaidia juhudi za serikali


Amesema katika kuitikia wito WA Mh Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akitoa fedha kwa makundi maalum kupata mikopo kwa ajili ya kuwania Wananchi kiuchumi

Aidha Bomboka ametumia fursa hiyo kuwaomba wanajamii kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Vitongoji ambao utafanyika mwezi UJAO, ili Kuwapa fursa Wananchi kuwachaguwa viongozi wanaowataka ili kuwaletea maendeleo

Awali Rais wa vikundi endelevu Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa YEMCO Vikoba Tanzania, Mohamed Basanga amesema Taasisi ya Yemco imekuwa ikijishughulisha na kusimamia vikundi vilivyoanzishwa Nchini.


Aidha basanga ameendelea kufanya majukumu mengine ya Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kuvitafutia fursa vikundi mbalimbali Tanzania ilikufikia Malengo yao ikiwemo masoko na mitaji kwa vikundi vilivyo Rasmi, ikiwemo kuvilea vikundi vilivyoanzishwa



Mmoja wa washiriki na pia washindi wa zawadi zilizotolewa,HALIMA Yahaya (Davina) amemshukuru kamati ya maandalizi ya Yemco kwa kutambua mchango wake katika kuanzisha vikundi Zaidi ya 150 Kutoka sehemu mbali mbali nchi ikiwemo mikoa ya ya nyanda za juu u hususani mkoa wa Iringa
Halima amesema kupitia Vikundi hivyo vya Yemco amepata manufaa mengi ikiwemo kukuza mitaji katika Biashara zake lakini kupanua wigo wa masoko ya Biashara zake ndani na Nje ya Nchi.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram