46 views 51 secs 0 comments

DKT SAMIA AIELEZEA DUNIA MKAKATI WA TANZANIA

In KITAIFA
November 02, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

-MAREKANI

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelezea dira yake ya kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika kupitia mikakati mitatu mikuu ya Serikali katika sekta ya kilimo.

Akiwa nchini Marekani jana aliposhiriki kwenye mjadala kuhusu kilimo barani Afrika katika mji wa Des Moines, Iowa, Rais Samia alisisitiza kuwa Serikali yake imejizatiti kukuza sekta ya kilimo ili kufikia lengo hilo.

Katika maelezo yake, Rais Dkt. Samia amebainisha mikakati mitatu muhimu ya kuendeleza kilimo ikiwamo uwekezaji katika Miundombinu ya Umwagiliaji.

“Serikali imepanga kuwekeza katika miradi mikubwa ya umwagiliaji ili kuhakikisha ardhi nyingi zaidi inakuwa na uwezo wa kuzalisha mazao kwa mwaka mzima. Hii inalenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kupunguza utegemezi wa mvua.

“Kuboresha Upatikanaji wa Teknolojia na Pembejeo za Kisasa: Ili kuongeza tija na ubora wa mazao, Serikali inashirikiana na wadau wa maendeleo kutoa teknolojia za kisasa na pembejeo kwa wakulima.

“Hii itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kupata mazao bora yenye thamani kubwa kwenye masoko ya ndani na nje. Kukuza masoko ya mazao ya kilimo

“ Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha mazao yanayozalishwa nchini yanapata masoko ya ndani na nje, na hivyo kuwapa wakulima faida zaidi kutokana na juhudi zao,” alisema Rais Samia

Rais Dkt. Samia alieleza kwamba kwa mikakati hiyo, Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika na hivyo kuchangia zaidi kwenye usalama wa chakula katika kanda nzima.

/ Published posts: 1575

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram