54 views 6 mins 0 comments

RAIS SAMIA KINARA MAPINDUZI NISHATI SAFI

In KITAIFA
November 02, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA


-DAR ES SALAAM

WIZARA ya Nishati imetoa rai kwa mashirika na wadau mbalimbali nchini wakiwemo Puma Energy Tanzania kuendelea kushirikiana kufanikisha azma ya Serikali ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo mkakati wa taifa wa nishati safi ya kupikia unaolenga asilimia 80 ya wananchi kutumia gesi ifikapo mwaka 2034 .

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa Tuzo kwa Mawakala wa Puma Energy Tanzania mwaka 2024,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.James Mataragio alisema bila shaka wadau katika sekta ya nishati na Watanzania kwa ujumla wanajionea  maendeleo na mapinduzi makubwa katika sekta ya nishati nchini ndani ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo anafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma na nishati za uhakika na gharama nafuu.

“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan  amekuwa akifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za nishati za uhakika na gharama nafuu. Rais amekuwa akifanya jitihada kubwa kuhakikisha mazingira na miundombinu ya sekta ya nishati inakuwa rafiki na bora kwa uwekezaji wa biashara pamoja na kuwafikia Watanzania wote bila kujali hali za vipato vyao.

“Jukumu letu sio tu kusimamia na kuratibu maendeleo ya sekta nzima lakini pia kujihusisha na wadau mbalimbali kupitia matukio kama haya kwasababu kwa namna moja au nyingine tunakutana na watumiaji wa nishati katika shughuli zenu za kila siku,” alisema Dkt Mataragio

Aisha alisisitiza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na miundombinu ya sekta ya nishati nchini ili kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma ya nishati .

Alisema moja ya jukumu la Wizara ya Nishati ni kuendelea kuhamasisha wadau kuweka mikakati ya kufanikisha nishati safi na wanachokifanya Puma Energy Tanzania ni mfano mzuri wa kufanikisha malengo ya Serikali ya kuwezesha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.

Kuhusu tukio la Puma Energy Tanzania kuandaa Tuzo kwa ajili ya mawakala na washirika wake Dkt. Mataragio  aliipongeza kampuni hiyo na kutoa rai kwa kampuni nyingine katika sekta ya nishati zinaiga utaratibu huo wa kuwakutanisha wadau wake kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu na kujadili muelekeo wa sekta ya nishati nchini.

“Matukio kama haya yanamchango mkubwa na ni afya kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu kwasababu mijadala inayatolewa na mrejesho halısı unaopatikana kutoka kwa walaji wa mwisho wa bidhaa  ambao ni wananchi unasaidia sana.

“ Tutafurahi endapo na sisi kutoka Serikalini ambao tunatembea na dhamira ya kutekeleza maono ya Serikali tunajukumu la kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi popote walipo.Hata hivyo mchango na ushirikiano wa wadau kutoka sekta binafsi ni jambo ambalo serikali inalithamini na kuendelea kudumisha ndani ya nchi yetu,” alisema Dkt.Matarajio aliyekuwa Mgeni rasmi katika utoaji wa Tuzo za Puma Energy kwa Mawakala wake kwa mwaka 2024.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dk.Seleman Majige amesema Puma onayomilikiwa kwa asilimia 50 na Serikali imekuwa na  mkakat mbalimbali na mkakati mmojawapo ni  nishati safi ambayo ni matumizi ya gesi.

“Na sisi kama Puma Energy Tanzania tumeshaanza mkakati wa kuuza gasi ya kupikia na mwakani kuanzia mwezi wa tatu tutaanza kuuza gesi ya kwenye magari katika vituo vyetu.Hivyo wananchi tujiandae kununua gesi katika vituo vyetu vya Puma Energy.

“Lengo letu ni  kupunguza foleni kubwa katika vituo vinavyofanyabiashara ya gesi ya magari na tunategemea kwa miaka inayokuja basi tutaenda mpaka mikoani. Niwaombe wananchi muendelee kutuunga mkono lakini na kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kama jinsi ambavyo anasisitiza suala la nishati safi,” alisema

Aliongeza kuwa soko la gesi ya magari ni kubwa na wananchi wengi wameitikia kwa kubadilisha magari kutoka kwenye kutumia petroli ua dizeli kwenda katika gesi.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah akizungumza tuzo hizo alisema kampuni yao inatambua umuhimu wa mawakala na washirika wao katika kufanikisha uendeshaji wenye mafanikio ya kufikia wateja na Watanzania kwa ujumla nchini kote.

“Shughuli hii inafanyika kila mwaka na hii ni mara nne ambapo mbali na hilo tunafahamu kutoa tuzo kwa wakala na wadau wetu ni kutambua mchango wao lakini pia kuimarisha mahusiano , kubadilishana mawazo kuhusiana na mwenendo wa utoaji huduma zetu na mustakabali wa maendeleo ya sekta ya nishati nchini kote

“Puma Energy Tanzania inajivunia kuwa na mawakala nchi nzima.Pamoja na hayo tutawndelea kuwa sehemu muhimu ya kuhakikisha kampuni yetu inaunga mkono jitihada za Serikali za upatikanaji wa huduma na bidhaa bora za nishati safi na tumejidhatiti kutekeleza dhamira ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kufanikisha kampeni ya nishati safi ya kupikia,”alisema Fatma Abdallah.

Aliongeza kuwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ndio kinara katika jitihada hizo ikiwa ni mkakati wa kuwasaidia wananchi wote kuhamia katika nishati safi ili kuepukana na madhara ya kiafya na kimazingira kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.

”Kwa pamoja Puma Energy tunaamini mkakati huu utafanikiwa na tayari tuna Puma Gas sokoni,” alisema

/ Published posts: 1575

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram