33 views 6 mins 0 comments

CCM MGUU SAWA SERIKALI ZA MITAA

In KITAIFA
November 05, 2024



Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amewataka wanachama wa CCM kutobweteka atika Uchagzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Kauli hiyo aliitoa jana Wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani hapa, ambapo aliwataka viongozi na wanachama kushikamana na kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi huo.

Pamoja na hali hiyo Makalla alisema kuwa wakati nchi ikielekea katika kameni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kila mwanachama ahakikishe hakuna kulala katika kutafuta ushindi wa chama hicho tawala nchini.

“Kwenye kipindi cha kampeni hakuna kulala wana CCM tuhakikishe tunapambana kutafute kura ili kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi kushinda kwa kishindo kwani Uchaguzi huu hakuna ile kushinda bila kupingwa japo kuwa kuna Mitaa, Vijiji na Vitongoji wenzetu hawajaweka watu.

“Pamoja na kwamba kuna dalili za wenzentu kutosimamisha wagombea kwenye maeneo mbalimbali itakapotea naomba niongee na wana CCM wa Kinondoni na nchi nzima kwamba uchaguzi huu hauna kupita bila kupingwa msibweteke kwani mmesikia chama fulani kimesema kitahakikisha hata kama CCM ndiyo wameteuliwa tutawapigia kampeni ya kupigiwa kura ya hapana,” alisema Makalla

Alisema katika uchaguzi huu hakuna ile kushinda bila kupingwa japo kuwa kuna Mitaa,Vijiji na Vitongoji vyama vya upinzani havijaweka wagombea.

“Pamoja na kuwepo kwa dalili za wenzetu kutosimamisha wagombea kwenye maeneo mbalimbali,Uchaguzi huu hauna kupita bila kupingwa msibweteke kwani mmesikia chama fulani kimesema kitahakikisha hata kama CCM ndio wameteuliwa tutawapigia kampeni ya kupigiwa kura ya Hapana,” alisema

CPA Makalla alisema CCM haitalala bali itahakikisha wanafanya Kampeni za kuhakikisha wanashinda.

‘”Chama cha Mapinduzi CCM kinatoa pongezi nyingi kwa wanaccm wote na wagombea wote kwa namna walivyojitokeza katika zoezi la kura za maoni,wagombea waliojitokeza katika nafasi mbalimbali ni zaidi ya 500,000 kwa nchi nzima na wana CCM walioshiriki kura za maoni nchi nzima ni zaidi ya milioni 10 katika kura za maoni,”alisema na kuongeza



‘”CCM imesimamisha wagombea katika kila Mtaa,vKijiji na Kitongoji nchi nzima,vhivyo tunayofuraha kwamba CCM haijaacha kitongoji hata kimoja, mtaa wala kijiji kote tumesimamisha wagombea kwa lengo la kushika dola na kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kishindo,” alisema

Alisema chama hakiwezi kushika dola kwa kusimamisha wagombea kwa baadhi  ya maeneo na mengine ukaacha hiyo inaonesha chama hicho hakipo tayari kushika dola.

CPA Makalla alisema kwa sasa kura za maoni tayari zimeisha hivyo wanaelekea katika  uteuzi wa wagombea wanaccm na watanzania wanaombwa kwenda kuwa kitu kimoja.

“Stori zote mitandaoni wakati wa kura za maoni ilikuwa ni CCM,vhuku vyama vingine havionekani,vila CCM  imeonyesha utaratibu wa kupata wagombea kwa njia ya demokrasia ila wenzetu hao walikaa kama fisi aliyekuwa anasubiri mkono uanguke na kila kura za maoni zilipoisha walikimbia kuangalia wapi wanapata.

‘”CCM imedhibitisha kwa vitendo kwamba ni chama cha demokrasia kilichoweka utaratibu wa kuwapata wagombea kwenda katika vyombo vya dola kwa maana uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu,” alisema

CPA Makala alisema baada ya kura za maoni CCM kama chama kilichopo madarakani na kinachoamini lengo la chama cha siasa ni kushika dola na kuanza kushika dola imeanza kwa mfumo wa uchaguzi wa Tanzania ni lazima ushinde Serikali za Mitaa na lazima ushinde Uchaguzi Mkuu.

“Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mingine nchini, CCM imefanya kazi kubwa ya hamasa ya uandikishaji na Mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri sana zoezi la uandikishaji zaidi ya watu milioni tatu waliandikishwa.

“Hamasa ile iliyotumika kujiandikisha hamasa hiyo  itumike kuomba watu kwenda kupiga kura muda utakapofika,” alisisitiza.

Alisema kujiandikisha pekee ake hakutoshi, walivyojiandikisha ndo wajitoe kupiga kura kwani msingi wa chama chao upo kwa mabalozi ambapo mabalozi walifanya kazi kubwa kuhamasisha  watu kujiandikisha hivyo pia wanauwezo wa kuhamasisha  watu waende kupiga kura muda ukifika.

“CCM inaamini uchaguzi wa Serikali za mtaa ni uchaguzi muhimu sana miradi ya maendeleo iwe zahanati, shule au kituo cha afya inajengwa katika mitaa au kijiji au kitongoji hivyo wenyeviti wa mitaa ni watu muhimu sana kwa kushirikiana na madiwani katika kuleta maendeleo,” alisema na kuongeza .

‘”Uchaguzi huu ni muhimu sana nyie mlioteuliwa mkaweke taswira nzuri, mmeaminiwa mkakisaidie chama pale mtakaposhinda mkaungana na madiwani pamoja na wabunge kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kuwaletea wananchi maendeleo,” alisema CPA Makalla

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu alisema siasa ni maisha kwenye kushindana kuna kushindwa, amewaomba wana CCM Wilaya ya Kinondoni kuwa na subira.

Akitolea mfano wake, Mtemvu alisema yeye alipata kura nyingi katika uchaguzi lakini hakushinda ila aliungana na mshindi aliyeshinda na kumpa ushirikiano wote hadi kutoa fedha na magari yake katika kampeni.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram