34 views 56 secs 0 comments

MRADI WA UFUNGAJI MIFUMO YA UMEME JUA 20,000 MBIONI KUANZA

In KITAIFA
November 05, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA



Imeelezwa kuwa, miradi ya ufungaji wa mifumo ya umeme jua ipatayo 20,000 ipo mbioni kuanza katika maeneo ya visiwani na makazi yaliyo vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala waย  Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy wakati wa kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Nishati na taasisi zake kilichoongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko jijini Dodoma hivi karibuni.

“Mradi huu unahusishaย  kufunga na kusambaza mifumo itakayozalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua katika makazi yaliyo vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa hasa visiwani kwa kufunga mifumo ipatayo 20,000 ndani ya miaka mitatu, ” Alisema Mha. Saidy

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram