136 views 36 secs 0 comments

BEI ZA MAFUTA MWEZI NOVEMBA 2024 ZAENENDELEA KUSHUKA

In BIASHARA
November 06, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

DODOMA: Bei za reja reja za mafuta kwa mwezi Novemba 2024 zimeendelea kushuka. Bei ya petroli kwa Dar es Salaam na Tangaย  imeshuka kwa asilimia 2.26 ambayo ni sawa na shilingi 68 kwa lita, huku Mtwara ikiwa imepungua kwa asilimia 2.16, ikilinganishwa na bei za mafuta za mwezi Oktoba 2024.

Aidha, bei ya dizeli pia imepungua kwa asimia 0.07ย  kwa Dar es Salaam, asilimia 0.17 kwa Tanga na asilimia 0.11 kwa Mtwara.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Novemba 6, 2024, imeeleza kuwa ahueni hiyo kwa bei za mwezi huu, inatokakana na kushuka kwa gharama za kuagiza mafuta ya petroli kwa wastani wa asilimia 3.91; na kupungua kwa
gharama za kubadilisha fedha za kigeni kwa wastani wa asilimia 1.75.

Kutokana na punguzo hilo, petroli mkoa wa Dar es Salaam itauzwa kwa shilingi 2,943 kwa lita, Tanga shilingi 2,948 na Mtwara shilingi 3,015. Kwa upande wa dizeli, bei za rejareja kwa mwezi Novemba 2024, Dar es Salaam ni shilingi 2,844 kwa lita, Tanga shilingi 2,855 na Mtwara shilingi 2,916.ย  Mafuta ya taa yatauzwa shilingi 2,943 Dar es Salaam, shilingi 2,989, Tanga na shilingi 3,016 Mtwara.

Ikumbukwe kuwa, bei za bidhaa za mafuta aina ya petroli zimeshuka mfululizo wa kipindi cha miezi mitatu, kuanzia mwezi Septemba 2024.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram