44 views 4 mins 0 comments

KILOGRAMU 1,066.105 ZA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA, MUUZAJI MAARUFU DODOMA ANASWA

In KITAIFA
November 12, 2024

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

KUFUATIA uchunguzi uliofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) imebaini baadhi ya wafanyabiashara wa shisha wanachanganya bidhaa hiyo na dawa mbalimbali za kulevya ikiwemo heroin ili kuiongezea radha na kupelekea madhara makubwa kwa watumiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo,Novemba 12,2024  wakati akitoa taarifa ya kukamata kilogramu  1,066.105  za dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa sugu wa dawa hizo Kamishna Mkuu wa DCEA Kamshna Aretas Lyimo amesema  kutokana na malalamiko mengi kuhusu kuongezeka kwa maeneo ambayo yanauzwa bidhaa hiyo na kuonekena imekuwa

“Utafiti tulioufanya mwaka mzima kwakuchukua  sampuli mbalimbali za shisha tumebaini baadhi ya maeneo wanachanganya madawa ya kulevya bangi,heroini na hashishi  zinachanganywa bila wahusika kujua ili kuleta hamasa kwa wavutaji,”amesema Kamishna Lyimo.

Amesema kutokana na hali hiyo wapo mamlaka ipo kwenye utaratibu      wa  kuhakikisha shisha inakuwa kwenye udhibiti  chini ya mamlaka hiyo.

“Shisha inatokana na mazao ya  tumbaku lakini watu wanayatumia  vibaya  wanaongeza vitu mwisho wa siku na wao watakuwa kwenye udhibiti,tutakutana na wenye bar wanaouza shisha na kuwapa elimu tutakuwa tunakagua na tunadhibiti kama ilivyo dawa nyingine za kulevya,”amesema Kamishna Lyimo.

Akizungumzia kuhusu kilogramu  1,066.105 za dawa za kulevya walizokamata  kupitia operesheni zilizofanyika katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Oktoba na Novemba 2024,amesema mbali na dawa hizo pia wamekamata mililita 447 za dawa tiba  zenye tiba zenye asili dawa ya kulevya na kuteketeza  jumla ekari 157 za mashamba ya bangi na lita 19.804 za kemikali bashirifu huku watuhumiwa 58 wakikamatwa katika operesheni hizo.

“Kati ya dawa hizo, kilogramu 687.32 za skanka na kilogramu moja 01) ya hashishi likamatwa eneo la Goba, Dar es Salaam, zikiwa zimefichwa ndani ya nyumba ya mtuhumiwa.

“Uchunguzi umebaini kuwa
wateja wengi wa skanka ni wanawake, ambao hudai kutumia dawa hizo kupunguza msongo wa mawazo na kujistarehesha. Skanka ni aina ya bangi yenye kiwango kikubwa cha sumu, inavyosababisha madhara makubwa kiafya,”amesema Kamshna Lyimo.

Amesema kuhusu, hashishi ambayo hutengenezwa kwa mchanganyiko wa maua na mafuta ya mbegu za bangi, inapovutwa huzalisha kemikali hatari zinazoweza kusababisha magonjwa ya akili kwa haraka,mara nyingi jamii huamini kuwa watu wanaopatwa na magonjwa haya wamerogwa,”amesema.

Amesema pia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mamlaka ilikamata milimita 120 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Codein, zikiwa zinasafirishwa kwenda nje ya nchini pamoja na millita 327 zilizokutwa nyumbani kwa muhumiwa eneo la Tabata Kinyerezi.

“Dawa hizo zilingizwa nchini kinyume na taratibu, zikiwa zimewekwa chapa bandia ya dawa za kuogeshea mbwa na paka ili kuepuka kubainika.

“Kukamatwa kwa dawa hizi ni ishara ya uwepo wa tatizo la matumizi holela ya dawa za tiba zenye asili ya kulevya, Hali hii inachangiwa na kuimarika kwa udhibiti wa dawa za kulevya na kusababisha wafanyabiashara na watumiaji kutumia dawa tiba ya kulevya kama mbadala wa dawa za kulevya,”amesema.

Kamishna Lyimo amesema katika mkoani Dodoma, Mamlaka pia imewakamata watuhumiwa wawili Suleiman Mbaruku Suleiman (maarufu Nyanda), mwenye umi wa miaka 52, na Kimwaga Msobi Lazaro (miaka 37) wakazi wa mtaa wa Kinyali, kata ya Viwandani.

“Watuhumiwa hao walikamatwa na jumla ya gramu 393 za heroin,Nyanda anafahamika kama kinara wa biashara ya dawa za kulevya mkoani humo na amekuwa akifuatilia kwa muda mrefu,”amesema.
Amesema  kupitia operesheni za kanda, DCEA pia imekamata kilo 303.553 za bangi, gramu 103.8 za heroin, na kilo 63 za mirungi katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mafanikio haya ni matokeo na nia thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha kuwa tatizo la dawa za kulevya linakomeshwa ili kulinda afya na usalama wa watanzania,”amesema Kamshna Lyimo.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram