56 views 2 mins 0 comments

BENKI YA BIASHARA TANZANIA (TCB) YAZINDUA
LIPA POPOTE KURAHISISHA MALIPO KWA
WAFANYABIASHARA

In BIASHARA
November 13, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

KWA mujibu wa ripoti ya uchumi ya mwaka 2023 inabainisha kuwa Asilimia 14 ya watanzania ndio wanaotumia huduma ya malipo ya lipa namba na QR code namba hiyo ikitajwa kuwa chini kutokana na makato ya miamala



Ili kurahisha shughuli za biashara kufanyika kwa urahisi benki ya TCB imetambulisha mfumo wa malipo wa lipa popote unaowezesha wafanyabiashara wa kati na wadogo kupokea malipo bila makato yeyote kwa wateja wao kutoka mitandao yote ya simu na benki.




Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja wadogo na wakati -TCB, Bi Lilian Mtali, wakati benki hiyo ikizindua huduma ya LIPA POPOTE ili kurahisisha ufanyaji wa miamala kwa wafanyabiashara hao amesema pamoja na mambo mengine huduma hiyo imekusudia kuleta ujumuishi wa kifedha hasa katika kupokea malipo moja kwa moja kwenye akaunti zao za benk



Jesse Jackson ni Afisa Mkuu wa huduma za kidijitali na ubunifu benki ya -TCB ameeleza kuwa takwimu zimeonesha kuwa asilimia 14 ya watanzania hutumia huduma ya lipa namba ambapo huduma ya LIPA POPOTE imelenga kuongeza uelewa ,matumizi ya malipo na kuchagiza ukuaji wa uchumi.



Aidha huduma hiyo imetajwa kushughulikia hitaji la malipo ya kifedha linaloongezeka kwa kasi nchini miongoni mwa wajasiriamali wadogo na wakati ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wa Taifa kwani huchangia asilimia 30 ya pato la Taifa huku benki ya biashara Tanzania -TCB ikitoa zaidi ya shilingi bilioni 300 ili kuleta ujumuishi wa kifedha katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo.



“LIPA POPOTE ni zaidi ya njia ya malipo ni hatua kuelekea uwezeshaji wa kiuchumi kwa
wafanyabiashara nchini, kuanzia mijini hadi jamii za vijijini. Lengo letu ni kuzifanya
huduma za kifedha ziwe salama, nafuu na zipatikane kwa watu wote,” alisisitiza Bw.
Jesse Jackson.



Kwa kuzindua suluhisho la kidijitali la malipo kama vile LIPA POPOTE, tunaboresha
kikamilifu malengo ya Tanzania ya kuongeza ujumuishi wa kifedha kwa
wafanyabiashara, watu binafsi na jamii ambazo hazijafikiwa bado. Njia hii ya malipo
inatarajiwa kubadilisha namna biashara ndogo zinavyofanya kazi, na kurahisisha

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram