Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC limeandaa kongamano la kuwawezasha wananchi kiuchumi ambalo litakalofanyika jijini dodoma disemba 3 na 4 Katika ukumbi wa eleki Ef
Kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali na mgeni rasmi Katika kongamano hilo ni waziri mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ambaye yeye ndio Mwenyekiti wa mkutano huo
Ameyasema hayo Leo Tarehe 16 NOVEMBA 2024 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng’i Issa Amesema kongamano hili la nane ambalo linalofanyika Kwa kila mwaka na dhima ya kongamano hili ni kufanya Tathimini ya utekelezaji maswala ya uwezeshaji hapa Nchini
Amesema kongamano ambalo linaloteta WADAU Kwa pamoja wanaotoka serikalini kama Mawaziri,Wakuu wa mikoa,Makatibu wakuu,Makatibu Tawala,wakurugenzi wa halmashauri na baadhi ya wakuu wa Wilaya na wadau wa uwezeshaji wa mifuko kiuchumi na wakuu wa makampuni mbalimbali vyama vya ushirika na wajawasiriamali mabenk na makampuni Kwa ujumla
“Sasa hivi tunautekelezaji wa miradi ya serikali kama SGR,Bomba LA mafuta na wakuu na wakandarasi ambao wanaoshughulika na miradi na wanashiriki Katika mkutano huo”. Amesema Issa
Ameongeza kuwa”Mkutano huo huwa tunatumia fursa Kwa kuzindua taarifa yetu ya Mwaka na kutoa Tuzo Kwa ambao waliofanya vizuri,huwa tunatuzo mbalimbali huwa tunatoa Kwa mikoa, Kwa kulinganisha mawizara,mikoa na taasisi mbalimbali ambazo zinazofanya ujasiriamali na wadau wengine ambao wamefanya ujasiriamali wao vizuri pia wanapata Tuzo”. Ameongeza Issa
Amebaimisha kuwa “Sisi Bado ni nchi ya kimasikini na wananchi Wetu wengi Bado wanajaribu kutafuta maisha Yao Ili wawe na uchumi mzuri,uwezeshaji tunaona jambo la msingi sana Kwa wananchi Wetu kuweza Kuendelea kiuchumi”
Mkutano huo unakadiliwa kuwa na watu Zaidi ya 500 Hadi 700 na kutokana na uzoefu ambao waliokuwa nao kawaida wanakuja watu kama hao pia fursa zitakazozalishwa pale ni kwanza watu kufahamu fursa zilizopo serikalini lakini vilevile na watu waliopata hizo fursa watu watakutana wafanyabiashara Wetu wa ndani wajawasiriamali wadogo na watu wanaotafuta fursa mbalimbali watakutana na watu ambao wamepata fursa
Kauli mbiu ya mkutano huo ni UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI NI MSINGI WA MAENDELEO YA WATANZANIA