Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Kaskazini Bw. Godbless Lema anatuhumiwa na baadhi ya wanachama wa Chama hicho Mkoani Arusha kwa kuongoza kwa Ubabe na kupandikiza watu anaowataka yeye kwenye Nafasi mbalimbali zinazowaniwa kwenye Uchaguzi wa kuchagua Viongozi mbalimbali wa Chama hicho Kanda ya Kaskazini.
Lema inadaiwa kuwa amekuwa akiwaweka wagombea anaowataka yeye kwa nguvu akijaribu kupanga safu yake kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025, akitumia Vijana wa Hamasa kuwapiga wale wanaompinga kwenye teuzi hizo za ndani ya Chadema pamoja na kuwasimamisha Viongozi wanaopishana naye mawazo.
Aidha wanachama hao kadhalika wameonesha kusikitishwa na maandalizi ya CHADEMA kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu wa 2025, wakishangazwa na namna ambavyo Chama chao kimeshindwa kusimamisha wagombea kwenye maeneo mengi kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa.