36 views 22 secs 0 comments

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEZESHAJI TAASISI ZA UMMA YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA BENKI YA TCB

In BIASHARA
November 17, 2024

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya uwezeshaji  Taasisi za umma imeridhishwa na utendaji kazi wa Benki ya Biashara Tanzania  -TCB, huku ikiielekeza benki hiyo kuendelea kutoa gawio kwa serikali kuu ili fedha hizo zitekeleze miradi mingine ya kimkakati.



Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam  Leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo Augustino Vuma wakati kamati hiyo ilipotembelea benki hiyo ili kufahamu mikakati, utendaji kazi pamoja na mwelekeo wake kwa mwaka 2025.

Amesema pamoja na mambo mengine ushirikiano wa benki hiyo na taasisi nyingine za serikali ikiwemo Shirika la Reli Tanzania -TRC, katika utoaji wa huduma imetajwa kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi nchini.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  -TCB, Adam Mihayo amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na Kijamii na kiuchumi

Itakumbukwa kuwa Kamati hiyo imekua ikifanya ziara yake ya kutembelea taasisi mbalimbali za Serikali ili kusikiliza changamoto zao, kuona utendaji wao wa kazi na kuwasilisha ripoti kwa serikali kuu.

/ Published posts: 1525

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram