Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro Mkoani Arusha wameonyesha kuwa na matumaini na Serikali kufuatia urejeshwaji wa huduma za kijamii ambazo zilikosekana kwa mda mrefu.
Hayo yamebainishwa leo Nov 18, 2024 na Mratibu wa mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) wakili Onesmo Olengurumwa ambapo amesema kwasasa Wananchi wa Ngorongoro wamedai kuanza kuthaminiwaa.
Amesema kupitia ziara waliyoifanya katika tarafa ya Ngorongoro wamebaini kuwa Wananchi wa eneo hilo wanamatumaini na Serikali kutokana agizo la Rais Samia juu ya urejeshwaji wa huduma za kijamii katika tarafa hiyo.
Wakili Onesmo amesema kuwa Wananchi wa kata Ngorongoro wamedai kuwa baada ya agizo la Rais Dkt. Samia walianza kuona baadhi ya viongozi wakianza kutembelea eneo hilo na kusikiliza changamoto zao hali ambayo kwasasa inawapa faraja na kujihisi kama watanzania wengine.
Aidha Mratibu huyo wa (THRDC) amesema kuwa licha ya ukarabati wa miundombinu ambao unaendelea kwa sasa, Serikali inapaswa kuanza kuongeza majengo mengine mapya.